Latest Posts

JAMII IMEASWA KUTUNZA VYANZO KUEPUSHA UKAME

Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu imetoa wito kwa wadau mbalimbali pamoja na jamii kuendelea kushirikiana katika uhifadhi na usimamizi wa rasilimali za maji kwaajili ya kizazi cha sasa na baadaye.

Hayo yamebainishwa na Meneja Mazingira Janeth Kisoma mkoani Morogoro wakati wakifanya usafi katika mto Morogoro ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa wiki ya maji ambapo amesema kuwa ni wakati sasa kutunza vyanzo hivyo ili kuepusha ukame kwa siku za mbeleni.

“Wadau na jamii wajue kila mmoja wetu anajukumu la kutunza rasilimali na vyanzo vya maji na kuwa endelevu kwaajili ya kizazi cha sasa na baadaye ili tu kuweza kuepusha ukame”, amesema Kisoma.

Pia Kisoma amewashukuru wadau mbalimbali kwa kwa kujitokeza katika kushiriki zoezi la ufanyaji usafi katika mto huo.

Nao baadhi ya wadau waliojitokeza katika zoezi hilo wamesema watashirikiana na Bodi hiyo katika kutoa elimu juu ya umuhimu wa uhifadhi wa vyanzo vya maji.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!