Latest Posts

JAMII YA KIFUGAJI YATAKIWA KUTUMIA ELIMU KUJIKOMBOA KIUCHUMI

Mlezi wa Umoja wa Wanafunzi wa Jamii ya Kimaasai wa Vyuo Vikuu na Kati mkoani Morogoro, Rickoyan Ole Ndung’ani amewataka wahitimu kutambua thamani ya elimu wanayoipata na kuitumia kama nyenzo ya kujikomboa kimaisha na kiuchumi kwani wengi wao wametoka katika familia masikini ambazo maisha yake yamekuwa yakitegemea ufugaji wa jadi kwa miaka mingi.

Ole Ndung’ani ametoa wito huo wakati wa kuwaaga wanafunzi wahitimu wa Vyuo Vikuu vya Morogoro wa Jamii ya kifugaji (kimaasai) ambapo amewasisitiza kuwa wazazi wao wameona umuhimu wa kuwekeza kwenye mradi muhimu wa elimu wakiamini kuwa huo ndio urithi pekee wa kweli walioweza kuwapa watoto wao.

Kwa upande wake Mwanasheria kutoka Jamii hiyo akaiasa Jamii ya Kimaasai kuacha tabia ya kuwaacha watoto wa kike katika elimu kwani kufanya hivyo ni kuwakosesha haki ya msingi

Naye katibu wa Chama cha Wafugaji Tanzania Mathayo Daniel amewataka vijana wa jamii hiyo kuuona uchaguzi kama ni fursa na kugombea katika nafasi mbalimbali katika kuleta maendeleo chanya katika jamii ya kifugaji

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!