Zaidi ya jamii ya waislam elfu moja wamefutulishwa na banking ya CRDB mkoani Mbeya lengo likiwa ni kusaidia watu wenye uhitaji na kujenga mshikamano kwa jamii katika mfungo huu wa mwezi wa Ramadhani.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Wakili Beno Malisa, Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Jaffari Haniu ameipongeza taasisi ya CRDB kwa hatua hiyo ya kuwasaidia wenye uhitaji, huku akitoa wito kwa viongozi na taasisi nyingine kujitokeza kusaidia jamii kabla mwezi huu wa mfungo wa Ramadhani kabla haujaisha.

Kwa upande wake Shekhe wa Mkoa wa Mbeya Safiri Ayasi ameipongeza CRDB na kuomba wadau mbalimbali kuunga mkono ujenzi wa shule ya sekondari itakayohudumia wananchi bila kujali dini.
Kwa upande wao viongozi wa dini na baadhi ya wanufaika wamewashukuru CRDB Bank kwa msaada huo wakisema chakula walichopatiwa kitawasaidia katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani huku Waislamu wakihimizwa kuendelea kutumia huduma za benki hiyo.
