Latest Posts

JUMIKITA: SERIKALI ISIINGIE KWENYE MTEGO WA KUFUNGIA MTANDAO WA X (TWITTER).

Baada ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) chini ya mwenyekiti wake Mohammed Ali Kawaida kuitaka serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuufungia mtandao wa X ambao zamani ulijulikana kama Twitter kwa madai kuwa mtandao huo unaruhusu mambo ambayo ni kinyume na utamaduni wa Watanzania, wadau wa habari wamekuja na maoni mseto kuhusu suala hilo.

Jumatano Juni 12, 2024 Jukwaa la Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) likiongozwa na mwenyekiti wake Shabani Matwebe limeiomba Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokukubali kamwe kuingia kwenye mtego wa kufungia mtandao huo wa kijamii.

“kama ilivyo Instagram, Facebook na YouTube, ‘X’ au Twitter ni sehemu ambayo vijana wa Kitanzania wamekua wakilitumia jukwaa hilo kujipatia riziki mfano matangazo lakini pia hata kazi nzuri za Serikali, wanahabari wa mtandaoni wamekua wakizichapisha X” Ameeleza Matwebe.

Matwebe ameeleza kuwa JUMIKITA iko tayari kushirikiana na serikali kujua namna bora ya matumizi ya mitandao ya kijamii na kutoa ushauri ili serikali isiingie kwenye mtego wa kufungia mtandao huo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!