Latest Posts

KAGERA YASHIRIKI KUMBUKIZI YA MASHUJAA NCHINI YASISITIZA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI

 

Theophilida Felician Kagera.

Mkoa Kagera umeungana na wananchi wengine hapa nchini kushiriki siku ya kumbukumbu ya mashujaa waliopambana na wanaoendelea kupambana ili amani ya nchi iendelee kuwa tulivu kama ilivyo kwa kipindi chote.

Akishiriki maadhisho hayo hii leo Tarehe 25 Julai 2024 mkuu wa mkoa Kagera Mhe Fatma Mwassa katika viwanja vya uhuru Mayunga Manispaa ya Bukoba amesema kuwa siyo kazi ndogo kuidumisha amani kwa miaka mingi hivyo ni muhimu watu wote kuwakumbuka mashujaa kwa kudumisha amani na utulivu.

“Niwapongeze wana Kagera wote kwa kipindi chote nimekaa Kagera naweza kusema katika sehemu zote nilizofanya kazi Kagera ni mkoa wa mfano kwa amani na utulivu hongereni sana, hata pale zilipotokea chokochoko flani flani watu wakagomea mambo fulani siyataji, vijana wangu na wafanyabiashara wangu wa Kagera waliendelea kuwa watulivu wakati wote hongereni sana na asanteni sana, yanayotokea nchi jirani tunayaona siyo mazuri natusishawishike kuyaiga wala tusitamani yakatokea karibu nasisi tuendelee na amani , upendo, mshikamano, katika mkoa wetu kwa ajili ya kuleta maendeleo”_Mkuu wa Mkoa Fatma Mwassa.

Kiongozi huyo ambaye ujumbe wake zaidi umejikita kuelezea juhudi za mashujaa hapa nchini hakusita kuwaelezea mashujaa waliopambana wakati wa vita ya uvamizi wa nchi jirani ya Uganda mwaka 1978-1979 wakitaka kuupora mkoa Kagera ili uwe sehemu ya nchi hiyo chini ya aliyekuwa Rais wakati huo Hayati Idi Amini Pamoja naye Rais wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Amefafanua kuwa mkoa Kagera ni mkoa pekee wenye historia ya kuguswa na vita hiyo ambayo madhara yake yaliwagusa moja kwa moja wana Kagera kwani wananchi waliuliwa, mali na baadhi ya maeneo yaliharibiwa pia.

Aidha amefarijika kuwaona baadhi ya mashujaa waliopigana vita hiyo kwenye viwanja hivyo jambo ambalo amelitaja kuwa ni la kujivunia.

Mkuu wa mkoa Mwassa amepewa heshima ya kuweka Ngao kwenye mnara wa mashujaa Mayunga hivyo ameahidi kufanya jitihada za kulikarabati eneo hilo ili kuendelea kuweka sawa kumbukumbu za mashujaa hao.

Hata hivyo baadhi ya viongozi akiwemo Kongozi wa JWTZ Mkoa Kagera Luteni Kanali Nimrod Ezekiel ambaye ameweka Sime kwenye mnara huo akifuatiwa na viongozi wa dini walioweka Mashada wamewaombea pumziko jema mashujaa waliokwishatangulia mbele ya haki huku wakiwatakia kheli na afya njema ambao wanaendelea na majukumu yakulilinda Taifa Akiwemo Rais Dkt Samia Suluhu Hassani.

Nao baadhi ya mashujaa wa vita ya Kagera wamepewa nafasi ya kusalimia nakuyaelezea mambo kadhaa jinsi walivyopigana hadi kumfurumusha Idi Amini na majeshi yake.

“Tuliokuwa kwenye mapambano tunawashukuru sana mliotufariji tukaenda na kurejea salama wakati, Mwalimu anatupokea pale Bunazi kulikuwa na Bendi moja ya Jeshi yalikuwemo maneno mawili moja linasema hivii! waliokufa walikufa kishujaa waliorudi tumerudi kishujaa, kwakweli vita ni mbaya inatisha! inatisha! tulivyovuka Mto Kagera ng’ambo ya pili tulishuhudia maiti zilizokuwa zimezagaa baada ya uvamizi wa Iddi Amini ilikuwa ni hali ya kutisha lakini tulikabiliana nayo tukamshinda mvamizi” mashujaa hao wakieleza bayana.

Hatahivyo wsmetoa wito wakiwasihi askari ambao wako katika majukumu kufanya kazi zao kwakutanguliza moyo wa kulipenda Taifa huku wakiipongeza serikali ya mkoa kwa namna ilivyowatambua na kuwashirikisha katika tukio hilo muhimu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!