Zaidi ya wananchi laki moja katika mikoa ya Geita na Kigoma wamenufaika na mradi wa KAGIS, uliolenga kuhamasisha elimu ya mtoto wa kike na kuwawezesha wasichana kurudi shuleni, huku sasa ukifikia tamati baada ya miaka mitano.
Akizungumza katika hafla ya kufunga mradi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Plan International nchini, Jane Sembuche, amesema utafiti wao umebaini kuwa watoto milioni tatu wenye umri wa miaka 7 hadi 17 wapo nje ya mfumo wa elimu. Amesema wasichana kutoka maeneo ya vijijini na familia zenye kipato cha chini ndio wanaoathirika zaidi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela, amesema mradi huo umehitimishwa ukiwa na mafanikio makubwa, ikiwemo kuibua changamoto zinazowakabili watoto wa kike na kusaidia wengi wao kutimiza ndoto zao za kielimu.

Baadhi ya wanufaika wa mradi wa KAGIS wameelezea manufaa waliyoyapata, wakisema umewasaidia kurejea masomoni na kuongeza uelewa kuhusu haki na fursa za mtoto wa kike.
Mradi huo uliotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano, umefadhiliwa na Serikali ya Canada