Mkuu wa Wilaya ya Kahama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri wa Mkoa wa Kikodi Kahama, Mboni Mhita ameipongeza Timu na Menejimenti nzima ya TRA Kahama inayoongozwa na Meneja wa Mkoa wa Kikodi Kahama Warioba Buhembere Kanire kwa ufanisi ambao wameendelea kuufanya na kuendelea kuongoza katika makusanyo.
Mboni ameipongeza TRA kwa ufanisi wa kuvuka lengo la makusanyo kwa asilimia 176.7 akieleza kuwa hayo ni matunda ya ushirikiano uliopo kati ya DC akiwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri wa Kodi, timu, Menejimenti ya TRA na walipa kodi wa Kahama.
Kahama ni moja kati ya wilaya zilizopo mkoani Shinyanga, ambayo ni mkoa maalumu wa kikodi na pamekuwa na kiwango kikubwa cha uhamasishaji wa kudai risiti katika maeneo mbalimbali ya kibiashara hali inayoelezwa kuchangia mafanikio hayo.