Latest Posts

KAMATI YA AFYA YATILIA MKAZO UMALIZIAJI HOSPITAL YA RUFAA GEITA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI imeitaka Hazina kuharakisha malipo kwa miradi ya ujenzi wa hospitali ili kuepusha ucheleweshaji unaoweza kusababisha miradi hiyo kusimama au kusua sua.

Akizungumza wakati wa ziara yake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Hassan Mtenga, amesisitiza umuhimu wa kukamilisha haraka sehemu ambazo bado hazijakamilika ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dkt. Mfaume Kibwana, ameeleza kuwa baadhi ya fedha zilizotolewa zimewezesha kuendelea kwa ujenzi wa hospitali hiyo, ingawa kuna maeneo yanayohitaji rasilimali zaidi ili kukamilika kwa wakati.

Mjumbe wa kamati hiyo, Ceci Mwambe, ameishauri serikali kuhakikisha ujenzi wa vikinga mvua unakamilika ili kuwasaidia wagonjwa. Akijibu hoja hiyo, Mhandisi kutoka Wizara ya Afya, Johnson Kamala, amesema ucheleweshaji wa ujenzi wa vizimba hivyo umetokana na sababu za kifedha na taratibu za manunuzi.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amesema wizara yake imepokea maelekezo ya kamati hiyo na itahakikisha maagizo yanatekelezwa haraka ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!