Latest Posts

KAMATI YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA, KILIMO NA MIFUGO YASHAURI WIZARA KUSAIDIAJUHUDI ZA MKOA WA MOROGORO

 

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imeelekeza Wizara ya Mifugo na Wizara ya Kilimo kuona namna ya kuisaidia Kamati hiyo kuusimamia vizuri Mkoa wa Morogoro katika kutimiza malengo yake kwenye sekta ya Kilimo na Mifugo.

Maagizo hayo yametolewa leo Machi 15, 2026 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Deodatus Mwanyika (MB) wakati yeye pamoja na wajumbe wa Kamati hiyo walipowasili Mkoani Morogoro kwa ziara ya siku moja.

Mwanyika amesema, maagizo hayo yanalenga kuusaidia mkoa huo kutokana na mikakati mizuri ya kilimo na Mifugo iliyo nayo pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa viongozi wa Mkoa huo katika kukuza sekta hizo mbili.

“mikoa ni mingi na mambo ya kutembelea ni mengi, siku zote tunategemea Wizara kufanyakazi……kuandaa kutembelea sehemu ambazo tunaona kabisa kuna potentials, Morogoro ni karibu… muone maeneo ambayo hata nyinyi mnataka sisi tusukume ndani ya Bunge na nje ya Bunge.” Amesisitiza Mhe. Mwanyika.

Aidha, Mwanyika amemhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kuwa Kamati hiyo itaendelea kushirikiana na Mkoa na kwamba wataendelea kuuona Mkoa huo kwa jicho tofauti kama walivyoahidi siku za nyuma.

Kwa upande wake Waziri wa Mifugo Bashiru Ally Kakurwa, amesema wizara yake inaendelea kujipanga katika masuala ya Miundombinu wezeshi mabwawa ya kudhibiti mafuriko, Afya ya mimea, na mengine mengi hu akisisitiza kuwa wanafanya hayo yote kwa ushirikiano na Wizara ya Kilimo.

Katika hatua nyingine Waziri Bashiru ameupongeza Mkoa wa Morogoro kwa kuanzisha Kampeni ya TUTUNZANE inayolenga kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji na kubainisha kuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia anatambua ubunifu huo na ameanza kuelekeza Mikoa yenye migogoro hiyo kuja Morogoro kujifunza kampeni hiyo.

Naye Waziri wa Kilimo Daniel Chongolo (MB) ameutaja Mkoa wa Morogoro kama Mkoa wa hifadhi ya chakula huku akibainisha kuwa wizara yake kwa sasa inapambana na tatizo la uingizaji wa mafuta ya kula hapa nchini na kwamba wako mbioni kupiga marufuku uingizaji wa mafuta hayo na badala yake wanahamasisha kilimo cha zao la michikichi.

Awali Mkuu wa Morogoro Adam Kighoma Malima aliieleza Kamati hiyo malengo ya Mkoa huo eneo la sekta ya Kilimo kuwa umejikita kwenye kilimo cha mazao ya kimkakati yakiwemo Kakao, Kahawa, Parachichi, Mchikichi, Karafuu na Korosho hivyo bado kunahitajika msaada wa Serikalini katika kushawishi taasisi za kifedha kuwekeza kwenye sekta ya kilimo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!