Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limefanikiwa kuwakamata watu watatu ambao wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya Hajrath Mshamo, mwanachuo wa mwaka wa tatu chuo cha mtakatifu Joseph kilichopo manispaa ya Morogoro kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali. Kamanda wa jeshi la polisi mkoa huo SACP Alex Mkama amesema kuwa, kwa kushirikiana na wananchi wamefanikiwa kumkamata,Tyson Oscar Eliakim (20) Elias Joktan Lenjement (29) pamoja na Fredrick Richard Nogwa (21) ambaye ndiye waliyewakodishia pikipiki watuhumiwa hao yenye namba za usajili MC.285 EDX Pia Mkama amesema vijana hao walitekeleza tukio hilo la kupora simu kwa lengo la kujipatia kipato na kupelekea kifo cha mwanachuo huyo, hivyo ametoa wito kwa wazazi na walezi kuweza kusimamia malezi pamoja na maadili ili vijana waweze kujipatia kipato kwa njia ya halali.