Latest Posts

KATIBU MKUU WA CCM ATOA WITO KWA VYAMA KUILINDA AMANI YA NCHI

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Emmanuel Nchimbi amewaomba wananchi na viongozi wa vyama mbalimbali kuendelea kuilinda amani ya nchi kwa wivu mkubwa, kupendana, na kupunguza chuki baina yao.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Nyankumbu, Geita, Balozi Nchimbi amesisitiza umuhimu wa mshikamano na amani katika jamii akisema kuwa bila amani, maendeleo hayawezi kupatikana.

“Ni jukumu letu sote kuhakikisha kuwa amani ya nchi yetu inalindwa. Tunapaswa kupendana, kushirikiana na kuepuka chuki ili kudumisha mshikamano,” amesema Nchimbi.

Pia, amewasihi viongozi wa vyama vya siasa kuweka masilahi ya taifa mbele na kuepuka migogoro isiyo ya lazima ambayo inaweza kuvuruga umoja wa kitaifa.

Balozi Nchimbi amehimiza wananchi kuendelea kuwa na uvumilivu na kutumia njia za amani kutatua tofauti zao.

Mkutano huo ulijumuisha viongozi mbalimbali wa chama na wananchi waliojitokeza kwa wingi kusikiliza ujumbe wa Katibu Mkuu, ambapo pia alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!