Latest Posts

KCCO YAKABIDHI VIFAA VYA MACHO VYA MILIONI 130.7 HOSPITALI YA RUFAA GEITA

Shirika lisilokuwa la kiserikali la Kilimanjaro Centre for Community Ophthalmology (KCCO) limekabidhi vifaa vya uchunguzi na matibabu ya macho, vikiwemo vifaa vya kusaidia upasuaji wa macho vyenye thamani ya shilingi milioni 130.7, kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita. Msaada huo unalenga kuwasaidia wananchi kupata huduma za afya ya macho kwa ukaribu zaidi.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita, Dkt. Mfaume Kibwana, amesema kuwa kupitia ufadhili wa KCCO wamefanikiwa kuwahudumia wanufaika zaidi ya mia nne, ambapo kati yao wagonjwa 54 walifanyiwa upasuaji wa macho.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa KCCO, Peter Kileo, amesema vifaa walivyovikabidhi vitasaidia kwa kiasi kikubwa utoaji wa huduma za upasuaji wa macho, huku akisisitiza kuwa lengo la shirika hilo ni kuendelea kusaidia huduma za kibobezi za afya ya macho nchini.

Wakati huohuo, baadhi ya wataalamu wa huduma ya afya ya macho mkoani Geita wameelezea namna wanavyoendelea kutoa huduma hizo pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo, ikiwemo upungufu wa wataalamu wa fani hiyo.

Kwa ujumla, msaada huo wa vifaa vya uchunguzi na matibabu ya macho kutoka KCCO unatarajiwa kuboresha kwa kiasi kikubwa utoaji wa huduma za afya ya macho katika Mkoa wa Geita, huku ukipunguza adha ya wananchi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo, na hivyo kuongeza fursa ya matibabu ya haraka na salama kwa wagonjwa wa macho.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!