Latest Posts

VIONGOZI WATAKIWA KUWA MFANO KWA KUFANYA MAZOEZI YA MWILI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohammed Mchengerwa, ameagiza viongozi wa mikoa, wilaya na halmashauri zote nchini kuhakikisha wanahamasisha watumishi wa umma na wananchi kushiriki kikamilifu katika mazoezi ya viungo ili kujenga afya bora na kuimarisha ustawi wa jamii.

Waziri Mchengerwa ametoa agizo leo Jumamosi Juni 14,2025  jijini Dodoma, aliposhiriki mbio za mazoezi (jogging) zilizofanyika katika eneo la Mtumba, akisisitiza kuwa ni muhimu kwa viongozi hao kuwa mfano kwa kushiriki moja kwa moja katika mazoezi na kuyafanya kuwa sehemu ya utamaduni wa kitaifa.

Mazoezi hayo yanalenga kupambana na magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari, shinikizo la damu na magonjwa ya moyo ambayo yamekuwa yakisababishwa kwa kiasi kikubwa na mtindo wa maisha wa kubweteka, hali inayochangia kupungua kwa nguvu kazi ya taifa.

Mbali na kushiriki katika jogging, Waziri Mchengerwa pia amejumuika na washiriki wengine katika zoezi la upimaji wa afya, ambapo amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila mtumishi wa umma kuhakikisha anapima afya mara kwa mara ili kubaini mapema changamoto za kiafya na kupata matibabu stahiki.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!