Latest Posts

KERO YA BARABARA MBEYA MJINI, MDAU AJITOKEZA KUKARABATI ITEZI

Na Josea Sinkala, Mbeya.

Ikiwa ni msimu huu wa masika (mvua) hali ya barabara katika baadhi ya maeneo mkoani Mbeya bado ni tete kutokana na kutopitika kwa urahisi hususani barabara za mitaa na barabara ndogo mitaani na vijijini licha ya juhudi za Serikali kuonekana kwenye baadhi ya maeneo kuboresha miundombinu hiyo.

Huko katika kata ya Itezi Uyole jijini Mbeya, wananchi na Serikali za mitaa zimeungana ili kuchangishana fedha kwa ajili ya kutafuta vifusi ili kufukia maeneo korofi ya barabara na kuzifanya zipitike vizuri.

Katika mpango huo wananchi na viongozi wao wa mitaa walipofika kwa mmoja wa wananchi katika mtaa wa Gombe Kusini kata ya Itezi, Samweli Katininda alIahidi kutoa mchango wake kuhakikisha maeneo korofi yote ya kata hiyo yanarekebishwa ikizingatiwa yeye ni mwenyekiti wa kamati ya elimu na mazingira mkoa wa Mbeya ndani ya jumuiya ya wazazi wa CCM.

Akizungumza na kituo hiki kuhusu mchango wake huo, Edeni Katininda amesema aliguswa na kuamua kugharamia ubebwaji kifusi kutoka nanenane na gharama ya mafuta ya gari ambalo pia ni la kwake, vibarua na dereva kuhakikisha wanafukia barabara zote za kata ya Itezi na maeneo mengine ya jirani huku akikana kuhusisha mchango wake huo na masuala ya siasa kuwa pengine ana dhamira ya kugombea nafasi yoyote kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

“Walikuja vijana ambao ni wa hapahapa mtaani (Gombe Kusini) baada ya siku kama mbili akaja mwenyekiti wa mtaa bwana Mandalasi akasema tunaomba mchango kiasi chochote ili kukarabati barabara zetu nikauliza gharama nikaambiwa ni kama elfu themanini kwa roli moja basi nikashauri tuunganishe nguvu bila kujali vyama vyetu tufanye kitu cha pamoja kwenye barabara zetu”, amesema Edeni Samweli Katininda na kuongeza;

“Mimi nafanya hivyo kwa kadri Mungu anavyonijalia na mimi nafasi yangu ni mwenyekiti wa malezi na mazingira mkoa wa Mbeya na Itezi tu sio mkoa naweza nikaenda Chunya ilimradi nina uwezo kwahiyo anayefikiri ninataka kugombea watu wanawezafikiri tu kwanza kwenye ubunge sisi hapa Mbeya mjini nikama walivyofanya Dodoma kwa mama Samia Suluhu Hassan, Mbeya hatuna mtu nje na Dkt. Tulia Ackson labda wapinzani ndio watafutage watu na kwenye udiwani kwamba labda nataka kata wanaojiuliza hivyo waende CCM mkoa waulize nafasi yangu watajua kwanini nafanya hizi”, ameeleza mdau huyo aliyejitolea kukarabati barabara kata nzima ya Itezi na baadaye maeneo mengine atakayoyafikia.

Baadhi ya wananchi na wajumbe wa Serikali za mitaa waliokutwa wakiendelea na kazi ya kushirikiana kufukia maeneo hayo korofi katika mitaa ya Gombe kusini na Mwasote kata ya Itezi wamemshukuru mdau huyo kwa kujitoa kuboresha barabara hizo kutokana na ukweli kwamba baadhi ya maeneo yamekuwa korofi kupita kawaida kiasi cha kusababisha usafiri kuwa kero zaidi hususani kwa wagonjwa na wajawazito.

Pamoja na mkakati uliopo na unaoendelea wa kujenga barabara ya njia nne katikati mwa jiji la Mbeya hadi Mbeya vijijini bado jiji hilo linakabiliwa na ubovu wa barabara katika maeneo mengi hivyo kutoendana na hadhi ya kuwa jiji la Mbeya hasa ukosefu wa barabara kubwa za kupunguza msongamano wa magari kwenye barabara kuu pamoja na zile za mitaani ambako nyingi bado ni barabara za vifusi na changarawe huku lami zikihesabika hasa katika kata saba za bonde la Uyole jijini Mbeya.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!