Latest Posts

KESI YA MPINA KUPINGA KUTOTEULIWA KUGOMBEA URAIS YAENDELEA MAHAKAMA KUU DODOMA

Kesi namba 21692 ya mwaka 2025 kupinga kutoteuliwa kwa Luhaga Mpina kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT Wazalendo katika Uchaguzi Mkuu ujao inaendelea kusikilizwa leo Mahakama Kuu, Dodoma.

Kesi hiyo imeibuka kutokana na uamuzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kumzuia Mpina kurejesha fomu, hatua iliyochukuliwa muda mfupi baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa kubatilisha uteuzi wake ndani ya chama.

Upande wa walalamikaji unawakilishwa na jopo la mawakili linaloongozwa na Wakili John Seka, huku upande wa INEC ukiongozwa na Vivian Method. Walalamikaji ni Bodi ya Wadhamini wa ACT Wazalendo pamoja na Mpina mwenyewe, na kesi hiyo inasikilizwa kwa njia ya mtandao mbele ya majopo ya majaji watatu: Longopa J, Kahyoza J na Kagomba J.

ACT-Wazalendo imeeleza kuwa uamuzi wa INEC unakwenda kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheria za Uchaguzi na haki za kiraia za mgombea. Chama hicho kimeiomba Mahakama kutoa amri ya dharura ya kusitisha utekelezaji wa uamuzi huo ili kumruhusu Mpina kuendelea na mchakato wa kugombea Urais.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!