Latest Posts

KITUO CHA KUSAMBAZA UMEME CHANUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO

Moto ambao bado haujafahamika chanzo chake umewaka na kuteketeza eneo la kituo cha kusambaza umeme mkoani Njombe
 
Kaimu meneja wa TANESCO mkoa wa Njombe Mhandisi Lazaro Bartazai mara baada ya kudhibiti moto huo amesema hakuna athari kubwa zilizojitokeza huku wakiendelea kufanya tathmini ya athari zilizopatikana.
 
“Kilichotokea mpaka tukakata umeme ni moto umeunguza maeneo ya store jirani na kituo chetu cha kusambazia umeme lakini haujaleta athari kubwa”, amesema Injinia Lazaro
 
Joel Mwakanyasa Mrakibu msaidizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji ambaye ni kaimu kamanda wa jeshi la Zimamoto mkoa wa Njombe amesema wakati tukio hilo likitokea tarehe 4 Septemba 2024, majira ya saa tisa na nusu alasiri walipokea taarifa kutoka kwa raia mwema juu ya moto kuwaka eneo la kituo na kufika mapema kuudhibiti moto huo.
 
“Tulikuta moto umeshaanza kuwaka lakini kwa kushirikiana naa wanachi pamoja na wafanyakazi wa TANESCO tulishirikiana kuuzima lakini chanzo cha moto hatujatambua chanzo”amesema Mwakanyasa
 
Aidha ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Njombe kuwa makini wanapochoma moto ili kutokuleta madhara ikiwamo kuchoma miundombinu iliyojengwa na serikali kwa gharama kubwa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!