Latest Posts

KONGAMANO LA KIMATAIFA LA HALAL KUFANYIKA DAR WIKI IJAYO

Kampuni ya MICO International Halal Bureau Limited, imeandaa kongamano la kimataifa la wadau wa Halal litakalofanyika siku ya Jumatano jijini Dar es Salaam.

Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Mohamed Matano amesema MICO ni kampuni pekee Tanzania ambayo inatoa ithibati ya Halal kwa wafanyabiashara na kampuni zinazotoa huduma ndani ya nchi.

“Tarehe 14 mwezi wa nane kutakuwa na kongamano la pili la kimataifa katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na tunatarajia kukutana na wadau wa Halal hapa nchini. Tanzania tuna nafasi kubwa ya kufanya Halal Industries katika utalii, katika dawa, famasia na fedha kwa hiyo tutakapokutana na wadau tutajadiliana namna ya kuboresha shughuli za Halal hapa nchini,” alisema.

Alisema wadau mbalimbali na viongozi wa serikali watahudhuria kongamano hilo la wadau wa Halal ambalo linakadiriwa kushirikisha washiriki 500 wanaofanya kazi kwenye kampuni mbalimbali.

“Kutakuwa na muda wa B2B yaani mtu mmoja mmoja kukaa na kuzungumza masuala mbalimbali ya Halal kwa hiyo tunaomba wananchi wote wanaopenda kushiriki kongamano hili wajisajili,” amesema.

Alisema MICO International Halal ndiyo inasimamia machinjio yote Tanzania kwa kuwafundisha wachinjaji mafunzo ya Halal na kuhakikisha machinjio hayo yanaendeshwa katika misingi ya Halal.

Amesema kampuni hiyo ilipewa idhini ya kuendesha shughuli hiyo na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!