Latest Posts

KULIPUKA KWA TESLA CYBERTRUCK KULIVYOGEUKA KUWA MATANGAZO YA BURE

Gari la Tesla Cybertruck ililipuka kwa moto nje ya Hoteli ya Trump International Las Vegas Jumatano, 01, 2024 huku ikimuua dereva na kujeruhi wengine saba.

Video zilizopigwa na mashahidi ndani na nje ya hoteli zilionyesha gari likilipuka na moto ukitoka ndani yake, huku likiwa limeegeshwa nje ya hoteli.

Afisa maalum wa FBI anayehusika katika upelelezi wa tukio hilo Jeremy Schwartz aliwaambia waandishi wa habari baadaye kwamba bado haijulikani kama mlipuko huo ulikuwa kitendo cha kigaidi.

“Najua kila mtu anavutiwa na neno hilo, na kujaribu kuona kama tunaweza kusema, hili ni shambulio la kigaidi. Hiyo ndiyo lengo letu na ndiyo tunachojaribu kufanya,” alisema Schwartz.

Aliongeza kwamba FBI ilikuwa imemtambua mtu aliyeendesha gari hilo, ambalo lilikuwa limekodishwa kutoka Colorado, lakini bado halikuwa tayari kutambulisha hadharani dereva huyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tesla Elon Musk alisema kwamba mlipuko huo hauhusiani na Cybertruck yenyewe. “Tumethibitisha sasa kwamba mlipuko ulisababishwa na fataki kubwa sana na/au bomu lililokuwa kwenye kitanda cha Cybertruck iliyokodishwa na halihusiani na gari lenyewe,”

Aliongeza kwamba Cybertruck na gari lililotumika katika shambulio la New Orleans vilikodishwa kupitia huduma ya kushiriki magari kutoka kampuni ya Turo.

Msemaji wa Turo alisema kampuni haikufikiria kuwa wapangaji wa magari waliokuwa wakihusika katika mashambulizi ya Las Vegas na New Orleans walikuwa na historia ya uhalifu ambayo ingewatambulisha kama tishio la kiusalama.

“Tunaendelea kushirikiana kwa karibu na mamlaka za usalama wakati wanachunguza matukio haya yote mawili,” alisema msemaji huyo.

Inasemekana kuwa kulipuka kwa gari hilo la Cybertruck mbele ya hoteli ya Trump ilikuwa ni mpango wa kuharibu sifa za magari hayo lakini pia kuvuruga biashara ya Trump.

Tukio hilo limegeuka kuwa karata ya matangazo ya bure kwa magari hayo kwani mlipuko ulikuwa mkubwa lakini madhara hayakuwa makubwa kwa nje kwani vitu vilidhibitiwa ndani ya gari.

Kupitia mtandao wa X na vyombo mbalimbali vya habari duniani zimekuwa zikitoka sifa njema huku watu wakitamani kununua gari hilo kwa sababu za kiusalama. Hata vyombo vya usalama vilieleza kuwa sehemu kubwa ya mlipuko ilidhibitiwa ndani na kutoka juu kwa kiasi kidogo.

Wakati kampuni ya Tesla imeanza kutoa magari ya Cybertruck ilisema kuwa yatakuwa ni magari salama na yenye uimara madhubuti hivyo kutokea kwa tukio kama hili ilikuwa kipimo cha sifa za magari hayo.

Mashuhuda na wanausalama wanaeleza kuwa hata vioo vya milango na madirisha ya karibu na ilipolipuka gari hiyo hayajaathirika kwa kiwango kikubwa.

Ikumbukwe mwaka jana wakati wa mchakato wa uchaguzi wa Marekani Elon Musk aliwekeza kiasi kikubwa cha fedha ili kumsaidia Donald Trump katika kampeni zake.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!