Latest Posts

KUTEKWA KWA KIONGOZI WA CHADEMA: POLISI WAANZA UCHUNGUZI

Jeshi la Polisi Tanzania limeanza uchunguzi kuhusu tukio la kutekwa kwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Taifa ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Ally Mohamed Kibao, lililotokea usiku wa Septemba 6, 2024.

Taarifa kutoka kwa msemaji wa Jeshi la Polisi, David A. Misime, zinaeleza kwamba tukio hilo lilitokea eneo la Kibo karibu na Tegeta wakati Kibao alipokuwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea Tanga kwa kutumia basi la Tashrif.

“Jeshi la Polisi, lingependa kutoa taarifa kuwa, lilipokea taarifa hiyo na kuanza uchunguzi wa kubaini kilichotokea, chanzo chake na watu waliohusika ni akina nani”, imeeleza taarifa hiyo.

Mchana wa siku ya Jumamosi Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika alieleza kuwa basi la Tashrif lilizuiwa na magari mawili yasiyokuwa na alama yoyote na atu waliokuwa ndani ya magari hayo walikuwa na silaha na walimchukua Kibao kwa nguvu.

Mnyika alitoa wito kwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) kujitokeza kutoa maelezo kuhusu tukio hilo, akisema kwamba bunduki zilizotumika ni aina ya zinazotumiwa zaidi na TISS kuliko Jeshi la Polisi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!