Latest Posts

LISSU KUSHIRIKI KESI MOJA KWA MOJA MAHAKAMANI, SIYO MTANDAONI TENA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imekubaliana na mapingamizi yaliyowekwa na mawakili wa utetezi katika kesi ya uchochezi na kuchapisha taarifa za uongo inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

Katika kesi hiyo inayohusiana na matamshi yaliyodaiwa kuchapishwa kwenye mtandao wa YouTube, mawakili wa Lissu wakiongozwa na Wakili Mpale Mpoki waliwasilisha mapingamizi wakipinga shauri hilo kuendeshwa kwa njia ya mtandao, wakisema kuwa njia hiyo inakandamiza haki ya mteja wao kushiriki kikamilifu kwenye mchakato wa usikilizwaji.

Katika maamuzi yake yaliyotolewa leo, Mahakama imekubaliana na hoja za mawakili wa utetezi na kuamuru kuwa kesi hiyo haiwezi tena kuendeshwa kwa njia ya mtandao. Badala yake, Magereza na upande wa Jamhuri wamelazimishwa kuhakikisha Tundu Lissu anafikishwa mahakamani moja kwa moja kila mara shauri hilo litakapotajwa au kuendelea kusikilizwa.

Shauri hilo lina makosa matatu, likihusiana na tuhuma za uchochezi na kuchapisha taarifa za uongo kupitia mitandao ya kijamii, hususan YouTube. Awali, serikali ilikuwa ikisisitiza kesi hiyo iendelee kwa njia ya mtandao licha ya upinzani kutoka kwa utetezi na mshtakiwa mwenyewe kuendelea kugoma kushiriki kwa mfumo huo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!