Latest Posts

lRC CHALAMILA AZINDUA KLINIKI MAALUM HOSPITALI YA MLOGANZILA

-Amshukuru Rais Dkt Samia kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya hapa nchini.

-Apongeza Hospitali ya Mloganzila kwa kubuni Kliniki maalum (Premier Clinic)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila Septemba 18, 2025 amezindua “Premier Clinic ” katika Hospitali ya Mloganzila Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo  RC Chalamila amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya Afya, kwa kuwa sasa Hospitali nyingi zina miundombinu mizuri, wataalamu wazuri, pamoja na vifaa tiba. ” Hakika huo ni uwekezaji mkubwa”

Aidha RC Chalamila ameipongeza Hospitali ya Mloganzila kwa kuwa wabunifu kuanzisha kliniki maalum (Premier Clinic) ambayo inakwenda kutoa huduma za kibingwa na ubingwa bobevu katika upandikishaji wa Figo, Uloto, nyonga, uchunguzi na matibabu ya ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu.

Vilevile upasuaji wa uti wa mgongo kwa watoto, matibabu ya saratani, huduma za upasuaji rekebishi, huduma za dharura na ajali, uchunguzi na matibabu ya mafuta kwenye mishipa ya damu pamoja na matibabu ya kisukari na Homoni.

Sambamba na hilo RC Chalamila amewataka wtumishi na viongozi kufanya kazi kwa bidii kwa ushirikiano kila mmoja ahakikishe anaacha alama ili kizazi na kizazi kimkumbuke

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!