Latest Posts

M/KITI UVCCM MARA: VIJANA ACHENI KUTUNISHA MISULI, FUATENI SHERIA

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mara, Mary Daniel, amewataka vijana kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuchafua taswira ya umoja huo na badala yake kuwa sehemu ya kutetea na kusaidia jamii ili kujijengea heshima.

Akizungumza na vijana wa Wilaya ya Tarime wakati wa kumalizia ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali mkoani humo, Mary amewataka vijana kuheshimu sheria na kuzingatia maadili wanapovaa sare za UVCCM.

“Mnapovaa hizo sare, acheni kutunisha misuli. Fanyeni kazi zenu kwa kufuata sheria, msijione kuwa mna haki kuliko wengine. Zingatieni maadili na miiko yenu mnapokuwa kwenye jamii zenu,” amesema Mary.

Aidha, amewataka vijana kuchangamkia fursa za mikopo zinazotolewa na serikali kupitia vikundi vya maendeleo kwa kuhakikisha wanaunda vikundi vyenye malengo yanayowawezesha kunufaika na mikopo hiyo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!