Kutokana na kuwepo kwa taarifa za upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii, hasa mtandao wa X, ikiwemo udukuzi wa akaunti za taasisi mbalimbali za Umma, Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) imetangaza kuanza kwa mpango wa mafunzo Maalum kwa Maafisa Ulinzi wa Taarifa binafsi (Data Protection Officers- DPOS) kutoka taasisi zote za umma na binafsi.
Akizungumza na Waandishi wa habari Alhamisi Mei 22,2025 Jijini Dodoma Kaimu Mkurugenzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Usajili na Uzingatiaji PDPC Mhandisi Stephen Wangwe amesema lengo la Mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo Maafisa hao na kuhakikisha taasisi zote nchini zinafikisha viwango vya kitaifa na kimataifa ya Ulinzi wa taarifa binafsi.