Latest Posts

MABOMBA YA SHILINGI MILIONI 700 KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI GAIRO

Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira wilayani Gairo Mhandisi Gilbert Isaack amesema kuwa mabomba yenye thamani ya shilingi milioni 700 yaliyotolewa wilayani humo kutoka serikalini yanakwenda kuboresha hali ya upatikanaji maji safi na salama wilayani humo ifikie asilimia 75.

Mhandisi Gilbert ameyasema hayo Juni 10, 2024 wakati akipokea mabomba hayo katika ofisi za RUWASA wilayani Gairo huku akisisitiza kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha wananchi wa mijini na vijijini waoishi wilayani humo wanapata huduma ya maji yenye uhakika.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wanaoishi wilayani Gairo wamesema kuwa wanaishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuboresha huduma ya maji kwani hapo awali walikuwa wanapata changamoto ya kutumia maji ambayo pia hutumiwa na mifugo hali ambayo imepelekea kuhatarisha afya zao.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!