Latest Posts

MACHINGA WAMSHUKURU NA KUMUOMBEA RAIS DKT. SAMIA

Machinga kutoka Mikoa mbalimbali Tanzania wamemshukuru na Kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia suluhu Hassan kwa namna anavyozipa kipaumbele na kuzitatua changamoto za Wamachinga nchini

Akizungumza kwenye kongamano la Machinga wa kariakoo la kumpongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia suluhu Hassan na kuombea Amani katika Taifa letu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais  ,Wabunge na Madiwani Wenyekiti wa Machinga Tanzania Steven Lusinde amesema serikali imeweka Mazingira wezeshi kwa wao   Kufanya Shughuli zao kwa amani

Lusinde amesema wameamua kufanya kongamano hilo ili kumshukuru Rais Dkt  Samia Suluhu Hassan hadharani kwani amewafanyia Mambo mengi machinga na hawana la Kumlipa Zaidi ya Kumshukuru na Kumuunga Mkono katika ajenda za Maendeleo

“Tutaendelea kufanya Makongamano haya Nchi nzima tutapita kila sehemu kueleza Mema  Ambayo Rais wetu Mpendwa Dkt samia Ametufanyia alisema Lusinde.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ya wilaya amesema serikali imetenga zaidi ya Bilioni 317 kwaajili ya Masoko huku akitumia nafasi hiyo kuwahakikishia wafanyabiashara ,Mamalishe na Bodaboda Pamoja na Makundi mengine ya wajasiliamali kuwa Ulinzi na Usalama wa Biashara zao ni wa Uhakika

Sekta ya Umachinga mbali ya Kutoa Ajira kwa makundi mbalimbali  pia inachangia Karibu asilimia 40 ya Pato la Taifa ( GDP )

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!