Latest Posts

MADENI YA WATUMISHI NA WAZABUNI SONGWE KAA LA MOTO, CHONGOLO ANG’AKA

 

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Daniel Chongolo, amewataka wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo kuhakikisha wanalipa madeni ya watumishi na wazabuni wanaowadai ili kutokwamisha utekelezwaji wa miradi ya maendeleo.

Akizungumza kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya maendeleo ya Mkoa (RCC) kilichofanyika mkoani Songwe kwa ajili ya kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026, Chongolo ameeleza masikitiko yake juu ya ucheleweshaji wa malipo hayo.

“Lipeni madeni ya watu, najua mlihitaji huduma hizi kwa sababu zilikuwepo kwenye bajeti, sasa hela ilienda wapi?”, amehoji RC Chongolo.

Mkuu huyo wa Mkoa amesisitiza kuwa wazabuni hao walitoa huduma kwa nia njema, lakini matokeo yake baadhi yao wameanza kukabiliwa na hali ngumu ya kifedha, ikiwemo kushindwa kulipa mikopo yao ya benki kutokana na ucheleweshewaji wa malipo yao kutoka Halmashauri hivyo kuagiza halmashauri zote kuhakikisha wanalipa madeni hayo kwa wakati ili kuimarisha uaminifu wa watoa huduma na kuboresha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Wakurugenzi katika mkoa wa Songwe wameahidi kuhakikisha wanalipa madeni hayo kwa wakati kwani mikakati mbalimbali imewekwa pamoja na ukusanyaji wa mapato ili kuendelea kujiimarisha kiuchumi katika Halmashauri zao.

Pamoja na mambo mbalimbali, wajumbe wa kikao hicho cha ushauri mkoa wameshauri mambo mbalimbali ya kufanyia kazi ili kupiga hatua zaidi kimaendeleo katika mkoa huo ikiwemo vyanzo vya mapato, kuwa na usimamizi thabiti wa miradi ya maendeleo na kuhakikisha miradi iliyoanza kuhakikisha inamalizika kwa wakati kwa maslahi ya jamii ambayo ndio walipa kodi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!