Wilaya ya Mbinga ni moja ya wilaya ambazo wananchi wake wanategemea kilimo katika kujikwamua kiuchumi ambapo madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga wameiomba serikali kuwawezesha fedha kwa wakati Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) ili waweze kutekeleza ujenzi wa barabara za vijijini ambazo zitawawezesha wakulima kusafirisha mazao yao kwa uhakika zaidi.
Wakiongea baada ya uwasilishaiji wa bajeti ya Wakala Wa Barabara Za Mijini Na Vijijini (TARURA) madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga wamesema kuwa asilimia kubwa ya wananchi wa halmashauri ya Mbinga ni wakulima huwa wanapata changamoto kubwa wakati wa kusafirisha mazao yao kutoka shambani hivyo wameiomba serikali kuwawezesha fedha TARURA kwa wakati ili waweze kutekeleza ujenzi wa barabara za vijijini.
Akiwasilisha bajeti ya TARURA mwaka 2026/2027 meneja wa TARURA wilaya ya Mbinga Mhandisi Oscar Musa amesema jumla ya shilingi bilioni 2.5 imetengwa kwa ajili ya maboresho ya barabara amabapo wanatarajia kufanya matengenezo ya barabara kilomita 74 ili ziweze kupitika misimu yote.

Halmashauri ya wilaya ya Mbinga kwa kushirikiana na TARURA imetenga bajeti ya kuboresha barabara ambazo zipo katika kata pamoja na vijiji hatua inayolenga kuimarisha miundombinu na kukuza uzalishaji wa mali.