Walimu wakuu kutoka Mkoa wa Mwanza na Shinyanga wakiwa katika siku ya mwisho ya mafunzo ya Uongozi na Usimamizi fanisi wa Shule yaliyoendeshwa na ADEM katika vituo mbalimbali vya Halmashauri ya Wilaya ndani ya Mikoa hiyo.
Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo walimu wakuu katika nyanja za uongozi, usimamizi na uendeshaji fanisi wa shule pia utawala bora katika mamlaka za Serikali za Mitaa na yamefanyika kuanzia tarehe 17-19 Septemba, 2024 katika Mkoa wa Kagera na Geita na katika Mkoa wa Mwanza na Shinyanga yamefanyika tarehe 21-23 Septemba, 2024.
Hii ni awamu ya tatu ya mafunzo hayo ambayo yatafanyika katika mikoa 13 ya Tanzania Bara ikihusisha jumla ya Walimu Wakuu 8,551 ambapo awali yamefanyika katika Mikoa 13 iliyohusisha Walimu Wakuu 9,132.