Latest Posts

MAFWELE: GOLUGWA ANACHUNGUZWA KWA MIENENDO YA KUSAFIRI KINYUME CHA TARATIBU

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kukamatwa kwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Amani Golugwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) mnamo tarehe 13 Mei 2025 majira ya saa 6:45 usiku.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo Faustine Mafwele siku ya Jumanne, Golugwa alikamatwa akiwa katika maandalizi ya kusafiri kuelekea Brussels, Ubelgiji, kupitia lango namba 03 (Terminal 3) la uwanja huo wa ndege.

Jeshi la Polisi limeeleza kuwa kukamatwa kwa kiongozi huyo wa juu wa chama cha upinzani kulitokana na “taarifa za siri kuwa amekuwa na mienendo ya kuondoka na kurudi Nchini bila kufuata taratibu za kisheria hapa Nchini.”

Kwa sasa, uchunguzi wa kina unaendelea ukishirikisha Vyombo vingine vya Usalama, huku Polisi wakiahidi kutoa taarifa zaidi kadri hatua zitakavyopigwa.

Jeshi hilo pia limewataka wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati hatua za kisheria zikichukuliwa.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati uchunguzi ukiendelea na kupuuza taarifa za upotoshaji kuhusu hatua hizi za kisheria zinazomhusu mtajwa,” inasema taarifa hiyo iliyosainiwa na Kaimu Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!