Latest Posts

MAHAKAMA YAMREJESHA WAKILI MWABUKUSI KUGOMBEA URAIS WA TLS, AAHIDI UTUMISHI ULIOTUKUKA

Wakili wa kujitegemea Boniface Mwabukusi amesema wakati anapata taarifa ya kuenguliwa kugombea nafasi ya Rais wa TLS (Chama cha Mawakili Tanganyika) na kamati ya rufani ya chama hicho yahakuamini kama Mawakili wenzake wanaweza kufanya dhulma ya aina hiyo dhidi yake kwa kuwa aliona wazi maamuzi hayo hayakuwa ya haki na hayakufuata misingi ya kisheria ndio maana hata wahusika hawakumpatia nafasi ya kujitetea

Wakili Mwabukusi amezungumza hayo leo, Ijumaa Julai 26.2024 mbele ya wanahabari muda mfupi baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam kutengua maamuzi ya kamati hiyo na kumrejesha Wakili Mwabukusi kugombea nafasi ya Rais wa TLS katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao.

Amesema imani yake ndio iliyomshawishi kukimbilia Mahakamani kwa kuwa aliamini wazi kuwa aliondolewa kwa ubabe na kwamba vitendo hivyo vilimkwaza kwa kiasi kikubwa ingawa alimini kuwa haki yake ataipata

Wakili Mwabukusi ameishukuru Mahakama chini ya Jaji Butamo Kasuka Philip (Jaji wa Mahakama Kuu, Masjala ndogo ya Dar es Salaam) kwa kuharakisha kesi hiyo ikizingatiwa kuwa kwenye mazingira ya kawaida ilipaswa iwe hivyo ili kwenda sambamba na tarehe ya uchaguzi husika

“Nawashukuru Mawakili wangu walifanya kazi usiku na mchana, nilisema tangu siku ya kwanza kuwa kwa vyovyote vile itakavyokuwa Mahakama imetusikiliza kwa haraka sana, kwa kuzingatia changamoto, na kwa kuzingatia muda, tuliahidiwa tufike leo saa tatu na sote ni mashahidi ilipofika saa tatu uamuzi ukaanza kusomwa” -Wakili Mwabukusi

Katika hatua nyingine, Wakili Mwabukusi amesema endapo atachaguliwa kuongoza chama hicho (Chama cha Mawakili Tanganyika -TLS) uongozi wake utakuwa shirikishi unaozingatia misingi ya sheria na utawala bora, na kwamba mara zote atakuwa mstari wa mbele kusimamia maslahi ya chama hicho na wanachama wake ili watimize majukumu yao kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu au taasisi yeyote kutoka ndani na nje ya TLS

Kwa upande wake Wakili Jebra Kambole aliyekuwa anamtetea Wakili Mwabukusi katika kesi hiyo sambamba na Mawakili wenzake 18 ametoa wito kwa mamlaka mbalimbali zinazotoa maamuzi nchini kutambua kuwa zina wajibu wa kuzingatia misingi ya kisheria katika maamuzi yao badala ya kutumia nafasi walizonazo kuumiza wengine.

“Mahakama imesisitiza kwamba mamlaka zinazofanya maamuzi mbalimbali ni lazima ziwe na mamlaka za kisheria zinazofanya maamuzi yao, kwa hiyo hayo tumeyapokea lakini pia tumeupokea uamuzi wa Jaji kwamba ile rufaa iliyokuwa imekatwa ambayo ilikuwa inamkosesha sifa Wakili Mwabukusi kuendelea kugombea kwenye uchaguzi wa TLS imefutwa, kwa hiyo tunashukuru sasa Mwabukusi anaenda kwenye box la kura” -Wakili Jebra

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!