Latest Posts

MAKALLA AMJIA JUU HECHE MAKAA YA MAWE KUPELEKWA NJE “HANA UTAALAMU WA UCHUMI”

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla, amemkosoa vikali Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, akimshutumu kwa kushindwa kuelewa masuala ya uchumi na biashara ya makaa ya mawe nchini.

Akizungumza Aprili 17, 2025 katika mkutano wa hadhara wilayani Masasi, mkoani Mtwara, Makalla amesema kauli za Heche kuhusu magari yanayosafirisha makaa ya mawe ni za kishabiki na hazina msingi wa kitaalamu.

“Jana nimemsikia rafiki yangu Heche analalamika kwamba magari yanasomba makaa ya mawe, anakutana nayo barabarani kwa maelfu, nikasema kwanza ushamba. Yaani kila gari lililobeba makaa ya mawe yeye anadhani linaenda nje ya nchi. Haya ni mambo yanayotaka ubobevu wa kuelewa biashara na uchumi, lakini hana taaluma hiyo,” amesema Makalla.

Makalla ameongeza kuwa makaa ya mawe ni fursa muhimu kwa maendeleo ya nchi kwani yanatumika katika viwanda vya ndani kama Tanga Cement na Wazo, pamoja na kuuzwa nje ya nchi ambako yanachangia mapato ya fedha za kigeni.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!