Latest Posts

MAKALLA: CHADEMA WAMEONA HAWANA USHINDI, WAKAAMUA KUPUMZIKA

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakina fursa wala mipango ya kuwanufaisha wananchi, zaidi ya maneno matupu na kampeni ya kuomba michango, na kwamba kimeamua kupumzika badala ya kushiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Akizungumza Aprili 13, 2025, katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Lindi Mjini, mkoani Lindi, Makalla amewataka wananchi waendelee kuunga mkono CCM akisema ndicho chama pekee kinachowaletea maendeleo ya kweli.

“Upinzani wakija hawaji na fursa yoyote zaidi ya bakuli na kofia wakisema ‘People’s Power’. Badala ya kusaidia wananchi, wanakuja kuomba mchango kupitia kampeni yao ya Tone Tone. Waambieni sisi tumepata shida na korosho lakini Dkt. Samia anatusaidia, mambo yetu yanaenda vizuri, wao waje na kejeli? Msiwape tena michango,” amesema Makalla.

Makalla alisema vyama vya upinzani vimepoteza mwelekeo, akitaja CUF na ACT-Wazalendo kuwa vipo kwenye hali ya kuyumba huku akidai CHADEMA wameamua kupumzika kwa kushindwa kuhimili mafanikio ya serikali ya CCM.

“CHADEMA wamepimaa, wamechungulia, wameona kazi zilizofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, wakatambua hawana ushindi, wakaamua kupumzika. Hawatakuwepo kwenye uchaguzi. CCM oyee!” ameongeza Makalla.

Amesisitiza kuwa hatua ya CHADEMA kushindwa kusaini makubaliano ya kanuni za maadili ya uchaguzi ni ishara kuwa hawatashiriki uchaguzi huo, na kwamba ni fursa kwa CCM kupata ushindi mkubwa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!