Latest Posts

MAKAMU MWENYEKITI UWT: CCM INAWATHAMINI NA KUWAJALI WALEMAVU

 

Makamu Mwenyekiti wa UWT Ndg Zainab Khamis Shomar(MNEC) ameongoza kongamano la wanawake wenye ulemavu wilaya ya Njombe lililofanyika katika ukumbi wa Johnson leo tarehe 29 Agosti 2024.

Kongamano hilo la wanawake wenye ulemavu limeandaliwa na wadau mbalimbali kwa kushirikiana na UWT wilaya ya Njombe likiwa na lengo la kuangalia na kujadili fursa zilizopo kwa walemavu, kuonesha uhodari wa utendaji wa kazi kwa walemavu, shughuli za ujasiriamali pamoja na kujadili namna ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili.

Makundi mbalimbali ya walemavu wakiwemo wanawake, wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za wilaya ya Njombe,wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi ( FDC) na wananchi wameshiriki kongamano ilo lililonogeshwa kwa burudani na maonesho yaliyoandaliwa na walemavu pamoja na uwasilishaji wa mada mbalimbali.

Akizungumza kwenye kongamano hilo Makamu Zainab ameeleza kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekuwa kikiandaa sera nzuri na wezeshi kwa wenye ulemavu nchini pamoja na utekelezaji wa miradi mbalimbali Kwa ajili ya walemavu kama shule maalum kwa ajili ya kupata elimu pamoja na uandaaji wa mikopo inayowawezesha walemavu nchini kuanzisha miradi inayowainua kiuchumi.

“Serikali ya CCM inawajali walemavu pamoja na kuwawezesha katika nyanja ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni, Serikali imekuwa ikitekeleza miradi ya elimu pamoja na utoaji wa mikopo kwa makundi ya walemavu”amesema Makamu Zainab na kuongeza

“Jumuiya ya UWT imekuwa ikiandaa nafasi kwa wanawake walemavu katika vyombo vya kutunga sheria kwa maana ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, lakini pia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi wamewateua watu wenye ulemavu katika nafasi za juu za Serikali”

“Chama na Serikali inawathamini na inatambua kama nyinyi ni watu muhimu katika taifa letu,na mimi niwapongezeni sana kwa jinsi mnavyojipigania na kujisimamia”

Akihitimisha kongamano hilo Makamu Zainab amekabidhi mahitaji mbalimbali ikiwemo chakula na nguo kwa wanafunzi walemavu wa shule za Kaparage, Kibena na Viziwi zote za wilaya ya Njombe.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!