Latest Posts

MALKIA WA NGUVU 7 WAPEWA TUZO KANDA YA KATI

Tuzo za Malkia wa Nguvu kanda ya Kati zimefanyika usiku wa tarehe 30 Agosti 2024 Jijini Dodoma kwenye ukumbi wa Mabeyo Complex na kuwatunuku Malkia 7 wa Nguvu kutoka Mikoa mbalimbali inayowakilisha Kanda ya Kati.

Washindi wa tuzo hizo kwa Kanda ya kati ni pamoja na Raha Aloyce kwenye tuzo ya Kilimo Biashara, Happy Augustino (Near Me) kutoka sekta ya Biashara ya Chakula, na Emeryciana Elikana Mbulagwisha (Ciana Event) kutoka Sekta ya Mapambo.

Wengine ni Ntegenjwa Hosea kutoka sekta ya Utumishi wa Umma, Mwalimu Sheila Hamis Chinja katika Mwanamke mwenye ushawishi, Ustawi wa Jamii kapata Hilda Kalisa, na Neema Silayo ambaye ameshinda tuzo ya Mjasiriamali Bora.

Kwa miaka minane Clouds Media Group imekua ikiandaa na kuratibu tuzo za Malkia wa Nguvu kwenye sekta mbalimbali ikiwamo sekta ya Chakula, Mapambo, Utumishi wa Umma, Kilimo, Mwanamke mwenye ushawishi, Ustawi wa Jamii na Mjasiriamali bora.

Mgeni rasmi, Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa amefurahishwa na hatua kubwa zilizopigwa na Clouds Media Group kwa kuhakikisha tuzo hizi zinafika mikoani badala ya Dar es Salaam pekee iliyokuwa ikifanyika miaka iliyopita.

Tuzo za Malkia wa Nguvu Kanda ya Kati zimehudhuriwa na watu mashuhuri mbalimbali akiwemo Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Babu Tale, Wabunge wa Viti Maalum Khadija Taya (Keisha), Nusrat Hanje, Catherine Magige, Mkurugenzi wa EFM na ETV Francis Cizar (Majizzo), Mtume Boniface Mwamposa na wengine wengi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!