Latest Posts

MAMA ALIYETELEKEZA MTOTO WA MWEZI MMOJA NJOMBE AKAMATWA

Zainab Abdalah (20) Mkazi wa Makambako Mkoani Njombe amepatikana na kukamatwa na Polisi kwa kosa la kutelekeza mtoto wa mwezi mmoja February 13 ndani ya ofisi ya kukatia tiketi kwenye moja ya kampuni ya basi mjini Njombe.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe limethibitisha kumkamata mama huyo ambapo katika mahojiano amebainisha kuwa sababu ya kumtelekeza mtoto wake ni kutokana na kushindwa kujikimu kimaisha yeye na mtoto wake baada ya kufukuzwa kwenye nyumba aliyokuwa amepanga katika mtaa wa Mji Mwema mjini Njombe.

Aidha Jeshi la Polisi limeeleza kuendelea kukamilisha uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hilo ili mtuhumiwa aweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Hata hivyo wito umetolewa kwa wananchi kuacha tabia ya kutelekeza watoto kwa kuwa ni kosa kisheria na kuitaka jamii au mwananchi aliyeshindwa kulea mtoto aweze kumfikisha kwenye vituo vya kulea watoto na sio kuwaacha mtaani wakiteseka.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!