Latest Posts

MAMA WA MIAKA (66) AELEZA ALIVYOWEKEZA MILIONI 14 AKITEGEMEA KUPATA MIL. 48 KWA MR. MANGURUWE/ USHAHIDI MAHAKAMANI

Kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mkondya (40), imeahirishwa mpaka Januari 30, 2026 baada ya shahidi wa 13 kutoa ushahidi na kuieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Es Salaam kuwa aliwekeza milioni 14 katika kampuni hiyo bila kupata matokeo.

Mkondya na mwenzake, Rweyemamu John (59), ambaye ni mkaguzi wa fedha wa kampuni hiyo, wanakabiliwa na mashtaka 28, yakiwemo kuendesha biashara ya upatu na utakatishaji fedha, huku mashtaka ya kutakatisha fedha yanayomkabili Mkondya pekee yake.

Kesi hiyo ina mashahidi zaidi ya 100 na leo shahidi wa kumi tatu aliyejitambulisha kama Sophia Watson Simtemvu Mkazi wa Makambako mkoani Mbeya, akiongozwa na wakili wa serikali Christopher alitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Beda Nyaki.

Anasema aliifahamu kampuni ya Vanilla International Limited mwaka 2021 kupitia matangazo yaliyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bwana Simon Mkondya(Mr/Dkt Manguruwe)

Anaeleza kuwa baada ya kuona matangazo hayo akashawishika kutaka kufanya kilimo biashara aliamua kutembelea ofisi za kampuni hiyo zilizokuwa eneo la TRA Njombe, ambapo alipokelewa na Gloria Mutabuzi ambae ni mfanyakazi wa kampuni hiyo kisha akaelezwa mazao mbalimbali yanayolimwa na kampuni hiyo.

“Vanila ni zao geni walituelekeza jinsi linavyozalishwa tukaondoka, tukarudi nyumbani tukapatana kama famila tukaridhishwa tulivuoona maelezo tukafunga safari mara ya pili kwenda ofisini tena.

Simulizi Kamili ya ushahidi ipo YouTube yetu ya Jambo TV hapa

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!