Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), mkoa wa Geita Manjale Magambo amewataka wanachama wa chama hicho kutokuruhusu watu kuwagawa kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji pamoja na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Manjale amesema hayo wakati wa shughuli ya kupandisha bendera za chama kwa mabalozi ambao wapo kwenye mtaa wa Kivukoni kata ya Kalangalala wilayani Geita, zoezi ambalo limeambatana na harambee ya ujenzi wa ofisi za CCM tawi la Kivukoni.
Amesema wanapoelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji pamoja na ule mkuu wa mwaka 2025 wanachama wanatakiwa kuwa wamoja na kuwapuuza watu ambao wamekuwa wakija kwa nia ya kutaka kuwagawa na kutumia vibaya jina la Rais Samia Suluhu Hassan.