Latest Posts

MAREKANI WALINYOOSHEA KIDOLE JESHI LA POLISI TANZANIA

Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umeeleza kuwa umeshtushwa sana na ‘taarifa za kuaminika’ kwamba polisi walitumia nguvu kupita kiasi wakati wa kuwakamata viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), washiriki vijana, na waandishi wa habari kabla ya mikusanyiko iliyopangwa kufanyika Mbeya katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Vijana.

Katika taarifa yake iliyotolewa Jumatano tarehe 14 Agosti 2024, Ubalozi huo umeeleza kuwa matumizi hayo ya nguvu kupita kiasi yalisababisha baadhi ya wanachama wa chama hicho cha upinzani kuumizwa vibaya na kuhitajika kulazwa hospitalini.

“Uhuru wa kujieleza, kukusanyika kwa amani, na haki ya kupata mchakato wa haki ni haki za msingi, na serikali zote zina jukumu la kudumisha misingi hii ya kidemokrasia. Tunaunga mkono wito wa mashirika ya Tanzania ya kiraia na tunaihimiza serikali ya Tanzania kuheshimu katiba yake, na kuhakikisha mazingira salama na wazi ya kisiasa ambapo sauti zote zinakuwa huru kushiriki”, umeeleza Ubalozi huo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!