Latest Posts

MBUNGE AGAWA MITUNGI YA GESI CCM KUHIMIZA NISHATI SAFI

Mbunge wa Jimbo la Momba, Condester Michael Sichalwe (Mundi), amegawa mitungi ya gesi 42 kwa viongozi wa Halmashuari kuu ya CCM kutoka kata 14 za Jimbo hilo, ikiwa ni juhudi za kuunga mkono kampeni ya Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kote nchini.

Mbunge Sichalwe, amesema zoezi hilo litakuwa endelevu, kwa kugawa gesi hizo kwa makundi mbalimbali kadri itakavyopatikana, lengo ni kuendelea kuhamasisha wananchi kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa kupikia na kugeukia matumizi ya nishati safi ili kutunza na kulinda mazingira na afya za wananchi.

“Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha matumizi ya nishati safi, na ndiyo maana Serikali imetoa ruzuku kwenye mitungi ya gesi ili wananchi wanunue kwa bei nafuu na kwa kuunga mkono jambo hilo, ndiyo maana na mimi nimeona nianze na ninyi wazazi wangu ili tunapo endelea kuwafikia na wengine ninyi muwe kielelezo muhimu”, amesema Condester Sichalwe, Mbunge wa Momba Mkoani Songwe.

Mbunge Sichalwe amesema miongoni mwa makundi yatakayofikiwa kupewa mitungi hiyo ya gesi bure ni pamoja na waheshimiwa madiwani wote wa Jimbo la Momba.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!