Latest Posts

MBUNGE AIOMBA SERIKALI KUWEZESHA WACHIMBAJI MGODI WA KIBAGA

‎Na Helena Magabe- Tarime

‎Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Michael Kembaki ameiomba Serikali kuwawezesha wachimbaji wadogo wa madini katika mgodi wa Kibaga Tarime ilinuendelee kuwanufaisha wakazi wa Tarime kwa kuchimba wenyewe kuliko kuchukuliwa na wawekezaji BARRICK GOLD MINE.

‎Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa jimbo Tarime mjini wa usonaji wa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM Mei 25,2025 alisema msimamo wake ni kwamba BARRICK wasinyemelee mgodi huo badala yake ni vema serikali iwawezeshe wachimbaji kwani mgodi huo unategemewa na watu wengi Tarime usichukuliwe na wawekezaji hao.

‎Alisema amefanikiwa kumaliza changamoto za wachimbaji wadogo wa mgodi wa kibaga waliokuwa na shida ya soko ambapo walikuwa wakitinza mawe kwa muda mrefu bila kupata soko huku wakitakiwa walipa mapato Halmashauri pamoja na TRA vile vile amefanikiwa kuondoa mapato hayo Halmashauri wanalipia TRA peke yake.

‎Alisema katika uongozi wake amefanikiwa kutatua migogoro sugu mitatu ya ardhi kwani kulikuwa na mgogoro wa Bugosi na Jeshi la Wananchi (JWTZ) ambao ulishindikana kwa muda mrefu lakini amefanikiwa kuumaliza baada ya Serikali kutoa fedha na wananchi wakalipwa fidia zao ,vile vile kulikuwa na mgogoro wa soko la Rebu ambao pia ameutatua umeisha  na mgogoro wa Mlima Nkongore ambao alida kitajengwa chuo kikuu mlimani hapo baaada ya mgogoro kuisha.

‎Akizungumzia sekta ya elimu alisema amejenga vyoo kwenye shule ya Tarime, Nyamisangura na Tagota  ,amenunua photocopy mashine kwenye kwenye shule mbali mbali alizozitaja  ,alifanikiwa kutengeneza madawati zaidi ya 1600 kwa kushirikisha WCF, NSSF,PSF pamoja na fedha za mfuko wa Jimbo vile vile amepunguza tatizo la kusoma kwa zamu kwa asilimia 80,vile vile kuanzi 2020-machi2025 zimejengwa shule mpya 7.

‎Alisema milioni 35,000,000 zilitumika kununua eneo la ujenzi wa sekondari sabasaba, 7,000,000 sekondari ya Nyamitende,10,000,000 shule ya msingi Ikohi ,17,000,000 kuezeka shule ya msingi Regoryo vile vile mchagiaji wa saruji mifuko 550 katika taasisi mbali mbali za shule 132,000,000. Na kuongeza kuwa kwenye sekta ya michezo, ufadhili wa Samia cup ulighalimu 146,000,000.

‎Kembaki alisema kwenye afya kulikuwa na changamoto ya vipimo hata vipimo vidogo wagonjwa walilazimika kwenda kutibiwa wilaya ya Rorya lakini kwa kushirikiana na Rafiki zake wa Sweden alinunua vifaa tiba vyenye thamani ya bilioni  1,200,000 kwa upande wa miundo mbinu ya barabara alisema wameweka taa 62  kuimalisha ulinzi na usalama na kutengeneza kilometa kadha za barabara mbali mbali  ambazo  alizitaja.

‎Hakusita kuzingumzia mradi wa maji wente thamani ya shilingi Bilioni  134 wa Ziwa Victoria mradi wa  Rorya,Tarime-Sirari ambao uko kwenye hatua za awali za utekelezaji ,vile vile ipo miradi mingine ya maji iliyotekelezwa na kukamilika ambayo imeghalimu 1,648,118,65.51.

‎Kwa upande wa Mwenyekiti wa CCM Wilaya Daudi Ngicho yeye alisema Waandishi wa habari  ni wapiganaji wa haki ,na haki ya kweli iko CCM alionya vikali Wazee wa mila kuingilia uchaguzi ndani ya chama kwa kutoa matamko aliongeza kuwa kazi yake ni moja kuhakikisha CCM iko salama Tarime na hayuko tayari kufanya kazi ya koo hata kama ana koo kwani alichaguliwa na Wanachama wa Tarime yote .

‎Katibu wa CCM Wilaya Hamza Kyeibanja alisema kuanzia januari 1,2025  hadi mei 25 ,2025 wamepokea Wanachama 2340 kutoka chama Cha demokrasia na maendeleo CHADEMA,ambapo katika mkutano huo walipokelewa Wanachama wawili Agnes Daudi toka kata ya Nkende pamoja na aliyekuwa katibu wa CHADEMA Sirari Mussa Mkiranda pia aliwahi kuwa katibu wa Vijana 2014-2019 alisema anarudi kwenye chama cha Familia na chama cha Baba.

‎Hata hivyo wajumbe wa mkutano walinufaika kwa kupata zawadi ya vikombe, chakula, pamoja na vitabu vilivyooanisha miradi mbali mbali iliyoanishwa na ghalama zake pamoja   na kutoa  shilingi 150,000,000 kwaajili ya nauli zao  huku  Walimu walimtunuku cheti Mbunge Mhe. Michael Kembaki.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!