Latest Posts

MBUNGE KOROGWE MJINI ATOA RAI YA KUIMARISHA UMOJA KATIKA MWEZI WA RAMADHANI NA KWARESMA

Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini, CPA Charles, ametoa rai kwa jamii pamoja na viongozi wa Wilaya ya Korogwe kutumia kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na Kwaresma kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii, ili kuimarisha umoja na kuleta maendeleo kwa wananchi.

Mbunge huyo ameyasema hayo wakati wa hafla ya Iftari iliyowakutanisha makundi mbalimbali ya jamii, wakiwemo viongozi wa dini, wananchi pamoja na wadau wa maendeleo. Hafla hiyo imelenga kuimarisha mshikamano, upendo na umoja wa jamii katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na Kwaresma kwa wananchi wa Jimbo la Korogwe Mjini.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, William Mwakilema, amesema serikali inaendelea kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa wilaya hiyo.

Amesema miongoni mwa changamoto hizo ni upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo mengi ya wilaya hiyo, lakini amebainisha kuwa mradi wa maji wa miji 28 unaoendelea kutekelezwa unatarajiwa kumaliza kabisa tatizo la maji wilayani humo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!