Latest Posts

MBUNGE NCHINI MAREKANI AVUTIWA NA UZURI WA TANZANIA

HABARI PICHA:

Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ameendelea kufanya mikutano na viongozi na wadau mbalimbali muhimu katika kukuza na kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Marekani. Miongoni mwa Viongozi hao ni Dkt. Ronny L. Jackson, Mwanachama wa Kamati Ndogo ya Afrika ya Bunge la Wawakilishi la Marekani.

Pamoja na masuala mengine, Mhe. Dkt. Jackson alimweleza Mhe. Waziri kuwa amewahi kufika Tanzania na anavutiwa na uzuri wa nchi, na pia anafikiria kuongoza Ujumbe utakaojumuisha Wabunge wengine kuitembelea tena Tanzania mwaka 2026 kufuatia mwaliko kutoka kwa Mhe. Waziri.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!