Latest Posts

MBUNGE NJEZA ATAMBA NA CCM KUSHINDA SERIKALI ZA MITAA

Na Josea Sinkala, Mbeya.

Mbunge wa jimbo la Mbeya vijijini Oran Manasse Njeza, amezindua kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa, vitongoji na vijiji katika Tarafa ya Tembela Mbeya vijijini na kuahidi kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitashinda kwa kishindo kutokana na utekelezaji miradi mbalimbali.

Akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Tembela, Mbunge huyo amesema Chama Cha Mapinduzi kina uwezo na ujasiri kuibuka kidedea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa kwani utekelezaji wa ilani umekuwa wa kuridhisha na kwamba vyama vya upinzani vinajisumbua kutokana na uimara wa CCM.

Njeza anasema katika jimbo lake (Mbeya vijijini) mambo mbalimbali yamefanyika ikiwemo uboreshaji miundombinu ya barabara, uimarishaji miundombinu ya elimu, mazingira ya utoleaji huduma za afy, usambazaji huduma ya umeme na maji vijijini na mambo mengine yanayoendelea kutatuliwa na Serikali iliyoundwa na chama hicho (CCM).

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Tembela Mhe. Juma Mwakalobo, ameishukuru Serikali kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali katika kata yake ulipofanyika mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa, vitongoji na vijiji unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!