Latest Posts

MBUNGE TARIME: WANANCHI MSIDANGWANYWE NA WANASIASA

Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Michael Kembaki amewataka wananchi wilayani humo kuacha kudanganywa na baadhi ya wananasiasa kuhusu utekelezaji wa miradi inayofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan badala yake wawe mabalozi kwa kazi zinazofanyika.

Kauli hiyo ameitoa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika stendi kuu ya mabasi Mjini Tarime mkoani Mara ambapo amesema wana chakujivunia kikubwa katika kazi kubwa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani humo katika sekta ya maji, elimu pamoja na barabara.

Pia katika hatua nyingine amesema ili kuhakikisha wanandoa changamoto ya ukosefu wa madawati katika halmashauri hiyo, tayari wamekwishatengeneza madawati 1000 ikiwa ni mkakati wa kuondoa changamoto hiyo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM, wilaya ya Tarime Mmkoani Mara Daudi Ngicho alisema Chama cha Mapinduzi katika Wilaya ya Tarime kitaendelea kufanya siasa za kistaarabu ambazo zitaenda sambamba na kutangaza kazi zinazofanywa na serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!