Latest Posts

MCH. MSIGWA: CHADEMA IDHIBITIWE KABLA HAIJALETA VURUGU NCHINI

Aliyekuwa kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) hivi karibuni Mchungaji Peter Msigwa amemshauri Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji (mstf) Francis Mutungi kuhakikisha anafuatilia kwa karibu vyama vya siasa vya upinzani nchini ili kujuwa namna vinavyoendesha mambo yao

Mchungaji Msigwa ametoa ushauri huo hivi karibuni akiwa kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika jimbo la Kawe, jijini Dar es Salaam ambapo ameeleza vyama hivyo alivyodai kuwa vinalenga kuleta vurugu nchini vimekuwa vikiendesha mambo yao kinyume na Katiba za vyama vyao zinavyotaka jambo ambalo amedai kuwa linapaswa kudhibitiwa

Akitolea mfano chama chake cha zamani (CHADEMA) Mchungaji Msigwa amesema kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamika kuwa Tume ya Taifa Uchaguzi (Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi) haiko huru, sambamba na kukosoa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini uhalisia uliopo ni kwamba viongozi wa chama hicho hawafuati hata Katiba ya chama chao jambo ambalo linapelekea wakose uhalali wa kukosoa Katiba ya nchi.

Amesema Katiba ya CHADEMA imeelekeza kuwa uchaguzi wa ngazi ya chini utasimamiwa na ngazi ya juu (yaani uchaguzi wa ngazi ya msingi utasimamiwa na tawi, uchaguzi wa ngazi ya tawi utasimamiwa na kata, uchaguzi wa kata utasimamiwa na jimbo, itaenda hivyo hadi kufikia ngazi ya Taifa) lakini viongozi wa chama hicho wakaamua kukengeuka Katiba ya chama chao na sasa chaguzi zinazofanyika ndani ya chama hicho zinafanyika kwa njia ya ‘oparesheni’ kwa kuwatumia maafisa walioteuliwa na makao makuu ya chama  wanaoitwa ZOC (Zonal Oparation Commander) ambao kimsingi hawajatwa popote kwenye Katiba ya chama hicho

Amesema amelazimika kuondoka kwenye chama hicho kwa kuwa hakuwa tayari kushuhudia akiendelea kutumika, kwani kwa muda mrefu amekuwa akikosoa sera na mipango ya CCM na serikali wakati ndani ya chama chao (CHADEMA) mipango na Katiba havifuatwi

“Katiba ya Chama cha Demokrasia (CHADEMA -Chama cha Demokrasia na Maendeleo) haifuatwi, nasema kwa ujasiri mkubwa kwa sababu nimekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama kwa takribani miaka 10 najuwa kinachofanyika” Amesema Mchungaji Peter Msigwa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!