Latest Posts

MCHINJITA: UCHAGUZI CHADEMA UMEONESHA DEMOKRASIA YA KWELI

Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Bara, Isihaka Mchinjita, amempongeza Mwenyekiti mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, kwa ushindi wake, akisema kuwa ni ushindi mkubwa katika mapambano ya demokrasia nchini.

Kupitia chapisho lake kwenye mtandao wa X, Mchinjita ameandika: “Hongera sana kwa ushindi Mh. @TunduALissu. Hakika huu ni ushindi wa mapambano ya demokrasia. Yako mengi ya kujifunza katika mapambano haya. Kipekee ninakupongeza na kukutakia kheri katika majukumu haya makubwa.”

Mchinjita amesisitiza kuwa ushindi wa Lissu ni wa CHADEMA kwa ujumla katika juhudi za kusimamia demokrasia ya kweli na kuhakikisha chaguzi huru na haki.

“Nampongeza pia Mwenyekiti anayemaliza muda wake Freeman Mbowe kwa kukubali matokeo na kumpongeza mshindi. Huu ni ukomavu mkubwa wa kisiasa,” ameongeza.

Aidha, Makamu Mwenyekiti huyo wa ACT Wazalendo amethibitisha nia ya chama chake kushirikiana na CHADEMA katika harakati za kuimarisha demokrasia nchini.

ACT Wazalendo tuko tayari kwa ushirikiano na mapambano ya pamoja kwa demokrasia ya nchi yetu,” amehitimisha Mchinjita.

Ushindi wa Tundu Lissu katika nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA umekuwa chachu ya mazungumzo nchini, ambapo wadau mbalimbali wamepongeza chama hicho kwa mchakato wa uchaguzi wa uwazi, huru, na haki.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!