Latest Posts

MCHINJITA WA ACT: WANANCHI WENYEWE WANATAKIWA KUCHUKUA HATUA KUDAI HAKI ZAO

Wananchi wametakiwa kuchukua hatua za kuanzisha mjadala wa kupambana na serikali iliyopo madarakani kwa kudai haki zao na kuboresha miundombinu mbalimbali kama shule, barabara na huduma za hospitali kutokana na malalamiko kwamba licha ya kulipa kodi za kutosha, maendeleo hayaonekani na wananchi wanahisi wanaishi katika hali ya ukoloni wa ndani.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo bara, Isihaka Mchinjita, tarehe 24 Julai 2024 katika kijiji cha Mwaipayi, kata ya Kilagano, jimbo la Peramiho mkoa wa Ruvuma akiwa katika ziara yake ya kutembelea mikoa sita ambayo aliianza tarehe 22 Julai 2024.

“Tunaomba vijana, watu wazima, na wazee mtuunge mkono kwa ajili ya vuguvugu hili la kupigania Tanzania mpya ambayo itajikomboa kama zilivyojikomboa nchi nyingine, kutoa vyama vilivyopo madarakani na vilivyokomboa uhuru wa nchi, ambapo sasa vinajigeuza wakoloni ndani ya taifa hili,” amesema Mchinjita.

Aidha amebainisha kuwa mkoa wa Ruvuma ambao unalisha Tanzania kwa kiwango kikubwa, unaongoza kwa udumavu wa lishe, ukosefu wa ajira, na shule bora za sayansi kwa vijana ambao ameutaja kuwa unatokana na “sera mbovu za Chama cha Mapinduzi (CCM)”.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!