Latest Posts

MFUMO WA TMX WAPAISHA MAPATO WILAYA YA MVUMERO

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro Judith Nguli amesema matumizi ya mfumo wa Soko la Bidhaa (TMX) katika uuzaji wa zao la Kakao umewezesha kupanda kwa bei ya zao hilo kutoka Tsh. 2,500 hadi 29,500 katika msimu wa mwaka 2023/24.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Agosti 14, 2024 amesema matumizi ya mfumo huo umekuwa neema kwa wakulima wa wilaya yake pamoja na Halmashauri kwa ujumla.

“Mfumo wa TMX kwetu umekuwa mkombozi, miaka mitatu iliyopita wakulima waliokuwa wanauza Kakao kati ya shilingu 1500 hadi 2500, lakini baada kuanza kutumia mfumo huu bei zilianza kupanda kati ya 7000 hadi 29,500.”Amesema Nguli na kuongeza,

“Katika msimu uliopita wilaya iliuza kilo miloni 3.3 na wakulima kufanikiwa kupata shilingi bilioni 44.7 na Halmashauri shilingi milioni 375.”

Nao baadhi ya wakulima wa zao hilo wamesema wanaridhishwa na usimamizi wa minada ya zao hilo ambayo imeendeshwa kwa njia ya Kieletroniki.

Tumaini Kelvin amesema mfumo huo wa TMX umekuwa mkombozi kwa wakulima kwani sasa wanapata fedha kwa wakati lakini umeongeza uwazi katika biashara yao kwakuwa wanashuhudia minada inavyofanyika.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!