Latest Posts

MGODI WA BARRICK NORTH MARA UNA TIJA KWA WANANCHI

Na Helena Magabe – Tarime

Licha ya kuwapo kwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya watu kwamba Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, uliopo Nyamongo wilayani Tarime, hausaidii jamii, baadhi ya wakazi wa maeneo yanayouzunguka mgodi wanasema mgodi huo umeleta manufaa makubwa kijamii na kiuchumi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Genkuru, Juma Elias Kegoye, Aprili 11, 2025, aliwaambia waandishi wa habari kuwa uwepo wa wawekezaji katika mgodi huo umekuwa na faida kwa wananchi tofauti na zamani ambapo rasilimali nyingi zilikuwa zinanufaisha watu wachache hivyo rasmali hiyo haikuwa na tija kwa Jamii.

Aliongeza kuwa kijiji cha Genkuru ni miongoni mwa vijiji 11 vinavyozunguka mgodi huo ,na Kijiji cha Genkuru kinanufaika kwa asilimia moja ya mapato kupitia fedha za mrabaha na akanti ya Kijiji cha Genkuru ina zaidi ya bilioni 2 pesa za Mrabaha .

Alisema awali, kabla ya mgodi kujenga wodi ya mama na mtoto, wanawake walikuwa wakipata shida kujifungulia hosipitali za mbali na amewahi kushuhudia mama aliyejifungulia njiani na baada ya kufikishwa kituo cha afya akakata roho.

Mtendaji wa Kata ya Nyarukoba, Frola Elias Magiga, alisema kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, kata hiyo ina wakazi 12,620 huku Kijiji cha Genkuru kikiwa na wakazi 5,664.

Aliongeza kuwa serikali ya kijiji imetenga fedha kwa ajili ya kununua kifaa cha upasuaji katika kituo cha afya ambacho ujenzi wake umekamilika, huku daktari akiwa kwenye mafunzo kwa vitendo.

Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Genkuru, Clinton Bernard Mligo, alisema ujenzi wa jengo la mama na mtoto umechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vya akinamama na watoto.

“Kwa sasa zaidi ya kina mama 46 hujifungua katika kituo hicho kila mwezi. Hata hivyo, bado kuna changamoto ya ukosefu wa jengo la kulaza wagonjwa na jengo la utakasaji,” alisema Mligo.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick North Mara, Apolinary Lyambiko, alisema mgodi unaendelea kutekeleza miradi mbalimbali yenye thamani ya shilingi bilioni 9.949.

Aidha, jumla ya shilingi bilioni 4.687 tayari zimepitishwa kwa ajili ya kuanzisha miradi mipya, ikiwemo upanuzi wa mradi mkubwa wa maji katika Kijiji cha Kewanja.

Pamoja na mafanikio hayo, Lyambiko alisema changamoto bado zipo, hasa katika msimu wa mvua ambapo wavamizi wa mgodi wameanza kujitokeza tena. Alitumia nafasi hiyo kuwaomba waandishi wa habari kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa mahusiano mema kati ya jamii na mgodi huo, ambao unaleta manufaa kwa wananchi na serikali kwa ujumla.

Meneja wa Mahusiano wa Mgodi huo, Francis Uhadi, alisema kupitia fedha za CSR, wamejenga jengo la mama na mtoto katika Kituo cha Afya cha Genkuru pamoja na barabara ya watembea kwa miguu (walkway), na kwamba lengo ni kuboresha miundombinu kwa ajili ya ustawi wa jamii.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!