News, Njombe.
Wakati wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji wakiendelea na zoezi la kunadi sera zao baada ya kuzinduliwa kwa kampeni nchini, mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa serikali ya mtaa wa Buguruni mjini Njombe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hekima Mhagama amesema licha ya ajenda alizonazo ili kuendeleza mtaa huo lakini akipata ridhaa ya wananchi kuongoza mtaa huo atakwenda kushirikiana na wananchi kupunguza kiwango cha udumavu kwa kutumia rasimali walizonazo.
“Mkoa wetu wa Njombe kuna mpango mkakati wa kutokomeza udumavu, sasa Njombe tumebarikiwa kuwa na kila kitu ikiwemo matunda lakini vitu hivi hatuvitumii ipasavyo, tutakwenda kutafuta wataalamu ambao watatusaidia kutupatia elimu ili tuweze kuzitumia rasilimali tulizonazo kuondokana na udumavu”, amesema Mhagama
Erasto ni mwenyeki wa Halmashauri ya mji wa Njombe ambaye pia ni diwani wa kata ya Utalingolo, akiwa mgeni rasmi katika kampeni hizo amewataka wananchi kuto kufanya makosa na kumchagua mtu mwingine nje ya mgombea wao kwa kuwa anao uwezo mkubwa wa kufanya kazi.
“Safari ya maono inaanzia kwenye shughuli yake, yeye ni mwalimu ana shule zake na shughuli zake zinaenda vizuri kwa hiyo kwa imani ile ile tunaimani atakapopewa madaraka maana yake kazi atazifanya vizuri kabisa”amesema Mpete.